Mufti: "Kuna umuhimu mkubwa wa kushirikiana katika kutibu tatizo la mmomonyoko wa maadili kwa njia za kielimu, kiroho na kijamii, ili kujenga Tanzania imara yenye watu wema, wakarimu na wenye tabia njema.
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA-
Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Dr. Abubakar Zubair bin Ally Wambwana, amefanya ziara muhimu ya Kitablighi na Kidini katika mkoa wa Iringa, ambapo ametembelea maeneo mbalimbali ya Kiislamu na Kijamii.
Miongoni mwa sehemu alizotembelea ni Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mheshimiwa Heri James, ambaye alimkaribisha kwa heshima kubwa na kufanya naye mazungumzo ya kina kuhusu masuala ya kijamii, hususan changamoto ya mmomonyoko wa maadili katika jamii.
Katika mazungumzo hayo, viongozi hao walisisitiza juu ya umuhimu wa kushirikiana katika kutibu tatizo hilo kwa njia za kielimu, kiroho na kijamii, ili kujenga Tanzania imara yenye watu wema, wakarimu na wenye tabia njema.
Your Comment